Yohane wa Kety (kwa Kipolandi Jan z Kęt au Jan Kanty) (23 Juni 1390 - 24 Desemba 1473) alikuwa padri wa Kanisa Katoliki, mwanafalsafa, mwanafizikia na mwanateolojia kutoka Poland.
Papa Klementi X alimtangaza mwenye heri tarehe 28 Machi 1676. Halafu Papa Klementi XIII alimtangaza mtakatifu tarehe 16 Julai 1767[1].
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 23 Desemba,[2][3] lakini pia 20 Oktoba.
Maisha
Alizaliwa Kęty, karibu na Oświęcim, Poland.
Baada ya kusoma chuo kikuu cha Kraków alipopata digrii mbili[4], mwaka 1418 alifikia udaktari wa falsafa.[5]
Miaka 3 iliyofuata alifundisha falsafa na kujiandaa kwa upadrisho.
Baadaye akawa gombera katika shule ya Wakanoni huko Miechow[5], akarudi Krakow kufundisha Sacrae Scripturae (Maandiko Matakatifu). Pia alipata udaktari wa teolojia na kuwa mkuu wa idara hiyo.
Yohane alitumia muda mrefu kunakili vitabu vya Biblia, teolojia n.k.
Katika fizikia, alisaidia kuendeleza theory of impetus ya Jean Buridan, akitangulia michango ya Galileo Galilei na Isaac Newton.
Huko Kraków, alijulikana sana kwa huruma na ukarimu wake kwa maskini, hasa wanafunzi wa chuo kikuu wenye shida. Alijipatia mahitaji halisi tu, ili kugawa mara kwa mara misaada kwa mafukara.
Mara moja alihiji hadi Yerusalemu na mara nne alihiji kwa miguu hadi Roma.[4]
Aliendelea kufundisha hadi kifo chake mwaka 1473, alipokuwa na umri wa miaka 83.
Tazama pia
Tanbihi
Viungo vya nje
Wikiwand in your browser!
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.