From Wikipedia, the free encyclopedia
Yeroboamu I (kwa Kiebrania ירבעם השני au יָרָבְעָם; kwa Kigiriki Ιεροβοάμ; kwa Kilatini Jeroboam) alikuwa mwana wa Nebati akatawala kwa miaka 22 Ufalme wa Israeli baada ya makabila 10 ya kaskazini kuasi ukoo wa Daudi wakati wa mjukuu wake Rehoboamu.
Biblia inamhukumu hasa kwa kuanzisha sera ya kidini iliyowataka Waisraeli wamuabudu YHWH kwa sura ya fahali ya dhahabu katika mahekalu ya Dani na Beteli ili wasiende Yerusalemu, mji mkuu wa ufalme wa ukoo wa Daudi
William F. Albright alikadiria ufalme wake kudumu tangu mwaka 922 KK – hadi 901 KK, wakati E. R. Thiele alisema kuwa alitawala tangu 931 KK hadi 910 KK.[1]
Agano la Kale linamtaja mara nyingi kama chanzo cha dhambi kuu ya Waisraeli ambayo hatimaye ilisababisha ufalme uangamizwe na Waashuru katika karne ya 8 KK.
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.