Wilaya ya Lushoto
From Wikipedia, the free encyclopedia
Wilaya ya Lushoto ni kati ya wilaya 11 za Mkoa wa Tanga nchini Tanzania.
Wilaya ya Lushoto ni sehemu ya milima ya Usambara. Inapakana na Wilaya ya Muheza na nchi ya Kenya upande wa kaskazini. Upande wa mashariki-kusini imepakana na Wilaya ya Korogwe. Upande wa magharibi imepakana na Wilaya ya Korogwe na Mkoa wa Kilimanjaro.
Mwaka 2012 ilikuwa na wakazi 492,441 walioishi katika kata 43 za wilaya hii. Katika sensa ya mwaka 2022 walihesabiwa 350,958 [1] katika tarafa 4, kata 29 na vijiji 118.