Werburga
From Wikipedia, the free encyclopedia
Werburga (pia: Wærburh, Werburh au Werburgh; Stone, Mercia, 650 hivi[1] - Trentham, Staffordshire, 3 Februari 699[2]) alikuwa malkia mdogo huko Uingereza.
Alianzisha monasteri kadhaa na hatimaye kujiunga na ile ya Ely ambayo ilianzishwa na kuongozwa na ndugu zake, akawa abesi wake baada ya mama yake, Mt. Ermenilda.
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.