Wayazidi
From Wikipedia, the free encyclopedia
Wayazidi ni kabila la watu wanaoishi hasa katika eneo la Kurdistan[1][2][3] na kwa namna ya pekee katika sehemu yake nchini Iraq[4][5], lakini wengine wengi wamekimbilia Ujerumani[6][7] na nchi nyingine.
Wanakadiriwa kuwa milioni moja au moja unusu.
Wanafuata dini yao maalumu ambayo inamuabudu Mungu mmoja tu. Kwa ajili yake wamedhulumiwa sana na Waislamu waliotawala eneo lao, kwanza Waarabu, halafu Waturuki.