![cover image](https://wikiwandv2-19431.kxcdn.com/_next/image?url=https://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/d/d8/Wangari_Maathai.jpg/640px-Wangari_Maathai.jpg&w=640&q=50)
Wangari Maathai
Mwanaharaki wa Mazingira na mwanasiasa aliyetuzwa tuzo ya Amani ya Nobel Prize Mwaka 2004. / From Wikipedia, the free encyclopedia
Wangari Muta Maathai (1 Aprili 1940 – 25 Septemba 2011) alikuwa mwanaharakati wa masuala ya mazingira na haki za wanawake kutoka nchini Kenya. Mwaka wa 2004 alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Amani.[1] Yeye ni mwanamke Mwafrika wa kwanza kupokea tuzo hilo. Pia, aliwahi kuwa mbunge wa Kenya na waziri msaidizi katika serikali ya Mwai Kibaki kati ya Januari 2003 hadi Novemba 2005.
![Thumb image](http://upload.wikimedia.org/wikipedia/sw/thumb/1/10/Tuzo_Nobel.png/320px-Tuzo_Nobel.png)
![Thumb image](http://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/d/d8/Wangari_Maathai.jpg/640px-Wangari_Maathai.jpg)
Katika maandalizi ya uchaguzi wa 2007 Maathai alisimama upande wa rais Kibaki lakini hakuteuliwa na chama cha PNU akagombea kwa chama cha Mazingira Green Party lakini hakurudi bungeni.