From Wikipedia, the free encyclopedia
Walter Frederick "Fritz" Mondale (5 Januari 1928 - 19 Aprili 2021) alikuwa mwanasiasa wa Marekani akiwa mwanachama wa Chama cha Kidemokrasia.
Makala haina vyanzo vya kutosha
Makala (au sehemu ifuatayo ya makala) inatoa habari bila kuonyesha vyanzo au uthibitisho wowote.
|
Kuanzia mwaka wa 1964 hadi 1976 alikuwa mbunge wa Senati ya Marekani akiwakilisha jimbo la Minnesota. Halafu alikuwa Kaimu Rais wa Marekani chini ya Rais Jimmy Carter kuanzia mwaka wa 1977 hadi 1981. Mwaka wa 1984 aligombea urais yeye mwenyewe lakini akashindwa na Rais Ronald Reagan.
Walter Frederick Mondale alizaliwa Januari 5, 1928, katika mji wa Minnesota,[1] wazazi wake walikuwa ni Theodore Sigvaard Mondale, na mama yake akiwa ni Claribel Hope (née Cowan), aliekuwa mwalimu wa muziki .[2][3][4] Mondale pia ana kaka ambao ni Clarence alikuja kujulikana kama Pete pamoja na Wiliam anaejulikana kama Mort, baba zao walihamia kutokea nchini Norwei,[5] Mondale alisoma katika chuo cha Macalester College kwa muda wa miaka miwili kabla ya kuhamia chuo kikuu cha University of Minnesota, na kupata shahada ya sanaa na astashada ya sayansi kaitka siasa mnamo mwaka 1951.[6] baaya ya Mondale kushindwa kujiandikisha katika chuo cha sheria aliamua kujiunga na jeshi mwaka huo huo wa 1951 muda mfupi baada ya kuwa amehitimu masomo yake.
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.