![cover image](https://wikiwandv2-19431.kxcdn.com/_next/image?url=https://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/c/c9/Victor_Wembanyama_Mets_92_%2528cropped%2529.jpg/640px-Victor_Wembanyama_Mets_92_%2528cropped%2529.jpg&w=640&q=50)
Victor Wembanyama
Mchezaji wa mpira wa kikapu wa Ufaransa / From Wikipedia, the free encyclopedia
Victor Wembanyama (amezaliwa 4 Januari 2004) ni mchezaji wa Ufaransa anayecheza mpira wa kikapu huko Metropolitans 92 ya LNB Pro A. Anakadiriwa sana kuchaguliwa na timu ya San Antonio Spurs kama chaguo nambari moja katika drafti ya Chama cha Mpira wa Kikapu Marekani (NBA) ya 2023 na anakadiriwa kuwa mmoja wa matarajio makubwa ya mpira wa kikapu wakati wote.[1][2][3]
![Thumb image](http://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/c/c9/Victor_Wembanyama_Mets_92_%28cropped%29.jpg/640px-Victor_Wembanyama_Mets_92_%28cropped%29.jpg)
Ni mzaliwa wa Le Chesnay, Ufaransa, Wembanyama alianza taaluma yake na timu ya Nanterre 92 ya LNB Pro A mnamo 2019. Miaka miwili baadaye, alihamia ASVEL na kushinda taji la Pro A katika msimu wake wa kwanza akiwa na timu hiyo. Mnamo 2022, Wembanyama alitia saini na Metropolitans 92 na kuchukua jukumu la uongozi. Amechaguliwa kuwa nyota wa LNB (All-Star) mara mbili, akishinda tuzo ya mchezaji mwenye dhamani zaidi katika mchezo wa nyota(mastaa) wa ligi ya LNB (All-Star Game MVP) mara moja, na ni Mchezaji Bora Chipukizi wa LNB Pro A mara mbili.
Wembanyama anachezea timu ya taifa ya Ufaransa ya mpira wa kikapu. Katika ngazi ya vijana, ameiongoza timu yake kutwaa medali mbili za fedha, ikiwa ni pamoja na Kombe la Dunia la FIBA chini ya umri wa miaka-19 2021, ambapo aliweka rekodi ya FIBA ya kuzuia kufungwa katika kila mchezo (blocks per game) kwenye shindano moja tu.