![cover image](https://wikiwandv2-19431.kxcdn.com/_next/image?url=https://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/3/3a/E._coli_Bacteria_%25287316101966%2529.jpg/640px-E._coli_Bacteria_%25287316101966%2529.jpg&w=640&q=50)
Usafi wa mazingira
From Wikipedia, the free encyclopedia
Usafi wa mazingira ni mbinu za kuzuia upanuzi wa maradhi hasa kwa kudhibiti majitaka na kinyesi pamoja na kupanga upatikanaji wa maji salama.
![Thumb image](http://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/3/3a/E._coli_Bacteria_%287316101966%29.jpg/640px-E._coli_Bacteria_%287316101966%29.jpg)
Taka ambazo zinaweza kusababisha matatizo ya afya ni kinyesi cha binadamu na cha wanyama, taka ngumu, maji machafu, taka za viwandani, na taka za kilimo. Hasa udhibiti wa maji taka na kinyesi ni muhimu kwa sababu viini vinavyosabisha magonjwa ya binadamu vinadumu katika vitu hivyo na kusababisha maambukizo kutoka mtu mmmoja kwa wengine.
Usafi kama njia ya kuzuia maradhi unaweza kutumika kwa ufumbuzi handisi (kama majitaka na tiba ya maji machafu), teknolojia rahisi kama vyoo, au matendo ya usafi binafsi (kama uoshaji wa mikono kwa sabuni).
Usafi wa mazingira kama unavyoelezwa kwa ujumla na Shirika la Afya Duniani (kwa Kiingereza World Health Organisation, kifupi WHO), unahusu utoaji wa vifaa na huduma ya usalama wa mkojo na kinyesi cha binadamu.
Upungufu wa usafi wa mazingira ndiyo sababu kuu ya maradhi duniani kote. Uboreshaji wa mazingira una manufaa makubwa kwa afya ya wote katika kaya na katika jamii.
Usafi wa mazingira unahusu pia udumishaji wa ratiba ya usafi, kwa njia ya huduma kama vile ukusanyaji wa takangumu na maji machafu.[1]