Uruguay (mto)
From Wikipedia, the free encyclopedia
Uruguay ni mto wa Amerika Kusini. Pamoja na mto Parana unaishia katika Rio de la Plata. Jina Uruguay linamaanisha "mto wa ndege ya rangi nyingi".
Ukweli wa haraka Mto wa Uruguay ...
Chanzo | milima ya Serra Geral (Brazil) |
Mdomo | Rio Plata |
Nchi | Brazil, Argentina, Uruguay |
Urefu | 1,790 km |
Kimo cha chanzo | takriban 1,800 m |
Mkondo | 4,622 m³/s |
Eneo la beseni | 370,000 km² |
Miji mikubwa kando lake | Concepción del Uruguay, Paysandu, |
Funga
Chanzo chake ni Brazil ya Kusini kwenye jimbo la Santa Catarina. Mwanzo wake ni mpaka kati ya majimbo ya Santa Catarina na Rio Grande do Sul ndani ya Brazil; baada ya mpaka kati ya Brazil na Argentina, halafu kati ya Argentina na Uruguay.
Jina la nchi ya Uruguay limetokana na mto huo na ni "Jamhuri upande wa magharibi ya mto Uruguay".
Meli haziingii sana ndani ya Uruguay kutokana na maporomoko yake.