nchi katika Amerika Kusini From Wikipedia, the free encyclopedia
Uruguay ni nchi ya Amerika Kusini upande wa mashariki ya bara kando ya Atlantiki.
| |||||
Kaulimbiu ya taifa: Libertad o Muerte (Uhuru au Mauti) | |||||
Wimbo wa taifa: Orientales la Patria o la Tumba! | |||||
Mji mkuu | Montevideo | ||||
Mji mkubwa nchini | Montevideo | ||||
Lugha rasmi | Kihispania | ||||
Serikali Rais |
Jamhuri Luis Lacalle Pou | ||||
Uhuru Ilitangazwa Ilitambuliwa |
25 Agosti 1825 28 Agosti 1828 | ||||
Eneo - Jumla - Maji (%) |
176,215 km² (ya 91) 1.5 | ||||
Idadi ya watu - Julai 2022 kadirio - 2011 sensa - Msongamano wa watu |
3,407,213 (ya 132) 3,286,314 19.8/km² (ya 206 1) | ||||
Fedha | Peso ya Uruguay (UYU ) | ||||
Saa za eneo - Kiangazi (DST) |
(UTC-3) (UTC-2) | ||||
Intaneti TLD | .uy | ||||
Kodi ya simu | +598
- |
Uruguay ni kati ya nchi ndogo kabisa za Amerika Kusini pamoja na Surinam.
Imepakana na Brazil na Argentina. Sehemu kubwa ya mipaka ya nje ni maji: mdomo mpana wa mto Rio de la Plata uko upande wa kusini-magharibi na Atlantiki upande wa kusini-mashariki.
Mji mkuu ni Montevideo wanapoishi zaidi ya nusu ya wakazi wote wa nchi (1,900,000 kati ya 3,407,000 hivi).
Wakazi wengi (87.7%) wana asili ya Ulaya, hasa Hispania na Italia. Wenye asili ya Afrika ni 4.6% na Waindio 2.4% tu.
Lugha rasmi na ya kawaida ni Kihispania.
Upande wa dini, nchi haina dini rasmi. Wakazi wengi (54.3%) ni Wakristo, hasa wa Kanisa Katoliki (44.8%).
Nchi na maeneo ya Amerika Kusini |
Argentina | Bolivia | Brazil | Chile | Ekuador | Guyana | Guyani ya Kifaransa | Kolombia | Paraguay | Peru | Surinam | Uruguay | Venezuela |
Makala hii kuhusu maeneo ya Uruguay bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Uruguay kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.