![cover image](https://wikiwandv2-19431.kxcdn.com/_next/image?url=https://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/c/c3/Drosera_spatulata_KansaiHabit.jpg/640px-Drosera_spatulata_KansaiHabit.jpg&w=640&q=50)
Umandejua
From Wikipedia, the free encyclopedia
Mimea ya Umandejua inaainishwa kwenye jenasi Drosera ambayo ni mojawapo ya jenasi kubwa zaidi ya mimea ambayo hula nyama. Jenasi ya Drosera ina angalau spishi 194[1]. Mimea hii ya familia ya Droseraceae huwavutia, kuwashika na kuwaua wadudu kwa kutumia viungo vyenye kuzalisha maji yenye gundi. Wadudu hawa hupendwa na umandejua kwa sababu mmea wenyewe unamea katika ardhi isiyokuwa na rotuba ya kutosha. Spishi mbalimbali, ambazo huwa na maumbo tofauti, hupatikana katika mabara yote isipokuwa Bara la Antaktiki.
Maelezo zaidi Uainishaji wa kisayansi ...
Umandejua | ||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
![]() Umandejua (Drosera tokaiensis) | ||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||
|
Funga