From Wikipedia, the free encyclopedia
Ufalme wa Aksum (pia: Axum) (kwa Ge'ez: አክሱም), ulikuwa milki muhimu katika karne za kwanza baada ya Kristo. Uliunganisha sehemu za nchi za leo za Ethiopia ya kaskazini, Eritrea, Sudan na Yemen. Mji mkuu Aksum uko katika Ethiopia ya leo. Milki hii ilianzishwa mnamo karne ya 1 KK ikaishia wakati wa karne ya 7 BK.
Hakuna uhakika juu ya vyanzo vya Aksum. Inatajwa kama milki muhimu katika Periplus ya Bahari ya Eritrea iliyoandikwa mnamo mwaka 70 BK. Wakati ule ilitawala tayari bandari muhimu ya Adulis kwenye pwani ya Bahari ya Shamu. Kutokana na bandari hii muhimu Aksum ilikuwa na nafasi ya kutawala sehemu ya biashara ya kimataifa kati ya Dola la Roma na Uhindi. Meli za nyakati zile zilikuwa jahazi zilizofuata pwani zikategemea bandari njiani na jahazi zote zilisafiri kati ya Misri ya Kiroma hadi Uhindi zilitegemea kituo cha Adulis.
Tangu kufifia kwa milki ya Kushi katika Sudan ya leo Aksum ilipanuka upande ule. Ilivuka pia bahari na kupanua eneo lake katika Uarabuni ya kusini sehemu za Yemen ya leo.
Chini ya Mfalme Ezana Aksum ilikuwa ya kwanza kubadili dini na kuwa Wakristo.[1][2]
Aksumu imetajwa katika karne ya kwanza katika Periplus of the Erythraean Sea kama sehemu muhimu ya masoko ya meno ya ndovu, yaliyokuwa yakitumwa katika sehemu mbalimbali duniani, chini ya Mfalme katika karne ya kwanza Zoskales ambaye pamoja na kuongoza Aksum, pia aliweza kuongoza pwani mbili za Bahari Nyekundu na (Assab) iliyopo nchini Eritrea; pia mfalme huyu anafahamika kuwa alikuwa na ujuzi fulani wa maandishi wa Kigiriki.[3]
Katika kipindi cha kupata mafanikio zaidi, Himata ya Aksum ilifanikiwa kujitanua hadi kufikia katika nchi inayojulikana sasa kama Eritrea, Kaskazini mwa Ethiopia, Yemen, Kusini mwa Saudi Arabia na kaskazini mwa Sudan.
Katika karne ya 3, Aksum ilianza kuingilia masuala ya ndani ya nchi kama vile Arabia ya Kusini, na mara kwa mara waliweza kuongoza Magharibi mwa mji wa Tihama. Pia iliweza kuongoza baadhi ya maeneo katika Peninsula ya Arabia na Bahari Nyekundu na kuwafanya walipe fedha kwa utawala wa Aksum.[4]
Katika mwishoni mwa karne ya 3, Aksum ilianza kutengeneza sarafu yake yenyewe na kuipa jina la Mani aliyekuwa moja katika ya mitume wanne wa kipindi hicho.
Hatimaye utawala wa Kiislamu ulifanikiwa kuchukua Bahari Nyekundu, na maeneo mengi ya Mto Nile na hivyo kuulazimisha utawala wa Axum, kujitenga katika shughuli za za kiuchumi.[4] Northwest of Axum (in modern day Sudan), Christian states of Maqurra and Alwa lasted till the 13th century before becoming Islamic.[4] Hata hivyo Axum ilibaki kuwa ya Kikristo.[4]
Katika sehemu ya pili ya golden age, hii ikiwa katika karne ya 6, utawala huu ulianza kuanguka na hatimaye kupoteza kabisa uwezo wake wa kuzalisha sarafu. Wakati wa kipindi hiki, wakazi wa maeneo ya Aksum, walilazimika kuingia ndani zaidi katika himaya hiyo kwa sababu za usalama. Historia za kijadi zinaandika kuwa, Malkia wa Kiyahudi, aliyejulikana kama Judith au "Gudith" aliiweza kuuangusha utawala wa Aksum, akachoma makanisa yaliyokuwapo pamoja na kumbukumbu za kiimaandishi. Lakini japokuwa tayari kuna ushahidi wa makanisa yaliyochomwa moto, bado suala la kuwapo kwa Malkia huyu katika eneo la Aksum, limeenedelea kujadiliwa siku hadi siku na waandishi mbalimbali.
Sababu nyingine ya kuanguka kwa utawala wa Aksum ni pamoja na Mabadiliko ya tabia nchi na kutengwa kimasoko. Matumizi ya ardhi kupita kiasi pia yalichangia ardhi katika maeneo hayo kushindwa kuzalisha mazao yenye rutuba na hivyo kushuka kwa uzalishaji wa mazao ya chakula. Pia hali hii ilisababisha na kubadilika kwa kutiririka kwa maji ya mto Nile na ukame.
Mazao makubwa yaliyokuwa yakitumwa nje ya Axum, yalikuwa zaidi mazao ya kilimo, kama vile shayiri. Watu wa Aksum hali kadhalika waliweza kufuga kondoo, ng'ombe na ngamia. Wanyama wakali walikuwa waliwindwa na kutoa vitu kama meno ya ndovu. waliweza kufanya kazi na wafanyabiashara kutoka Misri na Persia. Pia walikuwa na utajiri wa dhahabu na madini ya chuma, na chumvi.
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.