Trinidad na Tobago
From Wikipedia, the free encyclopedia
Jamhuri ya Trinidad na Tobago ni nchi ya visiwani katika Karibi ya kusini, karibu na pwani ya Venezuela, kusini kwa kisiwa cha Grenada cha Antili Ndogo. Nchi jirani nyingine kuvukia bahari ni Barbados na Guyana.
Ukweli wa haraka
| |||||
Kaulimbiu ya taifa: Together we aspire, together we achieve | |||||
Wimbo wa taifa: Forged From The Love of Liberty | |||||
Mji mkuu | Port of Spain 10°40′ N 61°31′ W | ||||
Mji mkubwa | Chaguanas | ||||
Lugha rasmi | Kiingereza | ||||
Serikali Rais Waziri Mkuu |
Jamhuri Paula-Mae Weekes Keith Rowley | ||||
Uhuru Kutoka Uingereza |
31 Agosti 1962 | ||||
Eneo - Jumla - Maji (%) |
5,131 km² (ya 165) Kidogo sana | ||||
Idadi ya watu - Julai 2019 kadirio - Msongamano wa watu |
1,363,985 (ya 151) 264/km² (ya 54) | ||||
Fedha | Trinidad and Tobago dollar (TTD ) | ||||
Saa za eneo - Kiangazi (DST) |
(UTC-4) (UTC n/a) | ||||
Intaneti TLD | .tt | ||||
Kodi ya simu | +1-868
- |
Funga
Nchi ina eneo la km² 5,128 ambalo karibu lote ni kisiwa kikuu cha Trinidad. Kile cha Tobago kina asilimia 6 tu za eneo pamoja na 4% ya wakazi. Kuna visiwa vidogo vingine 21.
Ni jamhuri mwanachama wa Jumuiya ya Madola.
Ni nchi iliyoendelea, ikishika nafasi ya tatu kati ya zile za Amerika baada ya Marekani na Kanada.