Tiberia
From Wikipedia, the free encyclopedia
Tiberia (pia: Tiberias; awali: Yam Ha-Kineret) ni mji wa Israeli kwenye pwani ya ziwa Galilaya, ambalo pengine linaitwa ziwa au bahari ya Tiberia (Yoh 6:1).
Mji huo ni maarufu kwa sababu Injili zinautaja kuhusiana na Yesu kuzidisha mikate na samaki kwa ajili ya umati (Yoh 6:23) na baada ya ufufuko wake kuwaandalia wanafunzi wake mikate na samaki juu ya makaa (Yoh 21:1).