From Wikipedia, the free encyclopedia
Thebes (kwa Kigiriki: Θῆβαι, Thēbai) ulikuwa mji katika Misri ya Kale karibu km 800 kusini mwa Bahari ya Mediteranea. Ilianza karibu na mji wa kisasa wa Luxor ikaendelea pia kwenye ukingo wa magharibi wa mto Nile ( 25.7° N 32.645° E ).
Thebai lilikuwa jina la Kigiriki, Wamisri wa Kale waliita Waset , ambayo ilikuwa pia jina la mkoa katika Misri ya juu.
Wakati wa Ufalme wa Kati, Farao Mentuhotep II alifanya Waset - Thebes kuwa mji mkuu wa Misri.
Hapo mahekalu makubwa yalijengwa au kupanuliwa ambayo yanaonekana hadi leo. Hasa mahekalu ya Karnak na Luxor hutembelewa na idadi kubwa ya watalii kutoka dunia yote.
Kwenye ukingo wa magharibi wa Mto Nile, wafalme walianza kujenga makaburi pamoja na mahekalu yao. Sehemu mashuhuri zaidi ni Bonde la Wafalme na hekalu la malkia Hatshepsut.
Thebes - Waset ilirudi kuwa mji mkuu mara kadhaa baada ya Mehutep II. Kuna uwezekano kwamba mnamo mwaka 1500 KK Thebes ilikuwa mji mkubwa zaidi duniani kwa wakati wake, ikiwa na wakazi 75,000[1]. Iliharibika wakati wa uasi dhidi ya mfalme Ptolemaio IX mnamo mwaka 84 KK; wakati wa Dola la Roma kikosi cha jeshi kilikaa katika hekalu la kale la Karnak. Mji wa Luxor ya leo ilikuwa kijiji kilichobaki kando ya hekalu la Luxor.
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.