![cover image](https://wikiwandv2-19431.kxcdn.com/_next/image?url=https://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/3/32/ApusBarbatus_TrevorHardaker2.jpg/640px-ApusBarbatus_TrevorHardaker2.jpg&w=640&q=50)
Teleka
From Wikipedia, the free encyclopedia
Teleka au barawai ni ndege wa familia Apodidae. Ndege hawa ni wadogo wenye mabawa marefu kwa umbo wa mundu. Rangi yao ni kahawia au kijivu na mara nyingi kiuno, koo na/au tumbo ni nyeupe. Teleka hupitisha takriban maisha yao yote angani wakikamata wadudu. Kwa hivyo ndege hawa hawawezi kutembea vizuri. Zamani watu walifikiri kwamba teleka hawana miguu, wakawapatia jina “apus” kutoka Kiyunani α = bila na πους = mguu. Hunywa pia wakiruka, lakini hulala wakishika nyuso ya wima.
Maelezo zaidi Uainishaji wa kisayansi, Ngazi za chini ...
Teleka | ||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
![]() Teleka mweusi | ||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||
| ||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||
Nusufamilia 2 na enasi 29:
| ||||||||||||
Funga
Teleka hujenga tago lao kwa vitu mbalimbali (vitawi, maua, majani, nyuzi, manyoya, wadudu) ambavyo vinagundishwa pamoja na mate. Matago ya spishi nyingine yamejengwa kwa mate pekee na haya yalika, huko Uchina hasa. Jike huyataga mayai 1-4.