Tabita wa Yopa (kwa Kiaramu טביתא, Ṭabītā, pia Dorkas, kwa Kigiriki Δορκάς, Dorkás[1][2][3]) alikuwa mwanamke Mkristo aliyeishi Joppa katika karne ya 1 BK.
Habari zake zinapatikana katika kitabu cha Agano Jipya kinachoitwa Matendo ya Mitume (9:36–42) .[4]
Humo tunasoma kwamba alikuwa anafuma au kushona nguo kwa faida ya mafukara, na hiyo inadokeza kwamba alikuwa na hali nzuri kiuchumi.[4] [5][6].[7][8]
Alipokufa, wafuasi wenzake wa Yesu walikwenda kumuita Mtume Petro katika mji jirani, Lydda, naye alipofika alimfufua.[8]
Anaheshimiwa na madhehebu mbalimbali ya Ukristo kama mtakatifu katika tarehe tofauti: 27 Januari[9], na hasa 25 Oktoba[9][10][11][9][12]
Tazama pia
Tanbihi
Viungo vya nje
Wikiwand in your browser!
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.