Sinodi ya maaskofu
From Wikipedia, the free encyclopedia
Sinodi ya maaskofu (kwa Kiingereza: Synod of Bishops) katika Kanisa Katoliki leo ni mkutano maalumu unaofanyika mara kwa mara ili kumshauri Papa kwa niaba ya maaskofu wote duniani. [1][2]
Maelezo zaidi Imani, Muundo ...
Funga
Sinodi hiyo ina sekretarieti ya kudumu mjini Roma.
Papa Fransisko ameendelea sera za watangulizi wake wa kuongeza mamlaka na athari ya sinodi hiyo katika Kanisa lote.[3] Kuanzia mwaka 2023 waumini kadhaa wasio maaskofu wala mapadri pia watakuwa na haki ya kupiga kura.