Sidoni Apolinari
From Wikipedia, the free encyclopedia
Sidoni Apolinari (jina kamili kwa Kilatini: Gaius Sollius Sidonius Apollinaris; Lyon, Galia, leo Ufaransa, 5 Novemba[1] 430 hivi - Clermont-Ferrand, 486) alikuwa mwanasiasa, mshairi[2][3], meya wa Roma na hatimaye askofu wa Clermont-Ferrand kuanzia mwaka 469 hadi kifo chake, ingawa aliwahi kuoa[4] na kuzaa watoto 4 [5].
![Thumb image](http://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/f/fe/SidonClermont.jpg/320px-SidonClermont.jpg)
Mwenye elimu kubwa katika mambo ya dini na ya dunia vilevile, kwa ushujaa wa Kikristo alipinga ukatili wa washenzi kama baba halisi wa wote na mwalimu maarufu [6].
Tangu zamani anaheshimiwa na Kanisa Katoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.