![cover image](https://wikiwandv2-19431.kxcdn.com/_next/image?url=https://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/4/40/Arles%252CSt_C%25C3%25A9saire27%252Cchoeur7%252CSt_C%25C3%25A9saire_%2528cropped%2529.jpg/640px-Arles%252CSt_C%25C3%25A9saire27%252Cchoeur7%252CSt_C%25C3%25A9saire_%2528cropped%2529.jpg&w=640&q=50)
Sesari wa Arles
From Wikipedia, the free encyclopedia
Sesari wa Arles (468/470 – 27 Agosti 542) alikuwa mmonaki huko Lerins, halafu Askofu mkuu wa Arles (Ufaransa) miaka 502 - 542.[1]
![Thumb image](http://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/4/40/Arles%2CSt_C%C3%A9saire27%2Cchoeur7%2CSt_C%C3%A9saire_%28cropped%29.jpg/640px-Arles%2CSt_C%C3%A9saire27%2Cchoeur7%2CSt_C%C3%A9saire_%28cropped%29.jpg)
Ingawa hakutaka kwanza kukubali cheo hicho, alijitokeza kuwa askofu bora wa nchi hiyo katika karne ya 6 akaacha maandishi mengi[2][3][4], zikiwemo hotuba zaidi ya 250 ambazo zisomwe na mapadri wakati wa kutoa katekesi kwa waumini na zilihusu hasa maadili katika jitihada zake za kufanya walei pia wafuate maisha ya kiroho kama wamonaki[5][6].
Ndiye aliyesimamia mtaguso wa Orange wa mwaka 529, ambao maamuzi yake yameeneza athari ya Augustino wa Hippo katika mafundisho ya Kanisa la Kilatini kuhusu neema ya Mungu[7].
Pia ndiye wa kwanza katika Ukristo wa Magharibi kuandika kanuni ya kitawa kwa wanawake (512) ili kuwaongoza katima maisha ya kimonaki, mbali na ile kwa wanaume [8].
Tangu kale anaheshimiwa na Kanisa Katoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu na babu wa Kanisa.