Sara
From Wikipedia, the free encyclopedia
From Wikipedia, the free encyclopedia
Sara (kwa Kiebrania שָׂרָה, Śārā, awali Sarai) katika Biblia anajulikana kama mke tasa wa Abrahamu ambaye kwa imani katika ukongwe wake alijaliwa kumzaa Isaka, baba wa Israeli, taifa teule la Mungu. Habari hizo zinapatikana hasa katika kitabu cha Mwanzo.
Jina lake linamaanisha mwanamke wa ukoo bora.
Tangu kale anaheshimiwa na Waorthodoksi wa Mashariki kama mtakatifu.
Waraka wa kwanza wa Petro unamsifu Sara kwa kumtii mumewe[1]
Waraka kwa Waebrania unamsifu kwa imani yake.[2]
Mtume Paulo anamtaja katika nyaraka zake kwa Wagalatia[3] na kwa Warumi[4] katika kueleza tofauti kati ya Agano la Kale na Agano Jipya.
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.