Sagara
From Wikipedia, the free encyclopedia
Sagara ni kata ya Wilaya ya Kongwa, katika Mkoa wa Dodoma, Tanzania, yenye postikodi namba 41503[1].
Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi walihesabiwa 28,536 [2]. Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 22,066 [3] waishio humo. Makabila yaishiyo Sagara kwa wingi ni Wakaguru na Wagogo.
Kata hii ina jumla ya vijiji 5: Sagara A na B, Msingisa, Ijaka, Laikala. Sagara ndiyo makao makuu ya kata ya Sagara. Kijiji cha Sagara kina mandhari nzuri kiasi, kina maji ya kutosha kutoka kwenye chanzo cha maji; wanakijiji hawanunui maji.
Katika kata za Sagara kuna shule za sekondari mbili na shule za msingi saba. mfano wa shule za msingi ni Sogelea, Sagara, Kadyango, Ijaka, Laikala na Msingisa. Shule Za sekondari ni Sagara na Laikala.