![cover image](https://wikiwandv2-19431.kxcdn.com/_next/image?url=https://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/e/e7/Kievan_Rus_in_1237_%2528en%2529.svg/langsw-640px-Kievan_Rus_in_1237_%2528en%2529.svg.png&w=640&q=50)
Rus
ukarasa wa maana wa Wikimedia / From Wikipedia, the free encyclopedia
Rus (Русь kwa Kirusi, Kiukraine na Kibelarus) ni eneo la kihistoria katika Ulaya ya Mashariki iliyokaliwa hasa na wasemaji wa lugha za Kislavoni likitawaliwa na familia zenye asili ya Skandinavia.
![Thumb image](http://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/e/e7/Kievan_Rus_in_1237_%28en%29.svg/640px-Kievan_Rus_in_1237_%28en%29.svg.png)
Watu walioitwa Warus walitokea Skandinavia na kufanya biashara katika Ulaya ya Mashariki kati ya Bahari ya Baltiki na Bahari Nyeusi hadi Mediteranea wakitumia mito kama njia. Walianzisha miji kadhaa wakafaulu kuunganisha au kutawala makabila ya Waslavi walioishi katika maeneo hayo[1]. Waliunda milki kadhaa zilizostawi kuanzia karne ya 9 hadi kuja kwa Wamongolia katika karne ya 13.
Milki kubwa zaidi ilikuwa Rus ya Kiev na mtawala wake aliamua kupokea Ukristo wa Kiorthodoksi mnamo mwaka 988[2]. Katika karne ya 11 milki mbalimbali ndani ya Rus zilianza kupigana kati yao. Baada ya uvamizi wa Wamongolia, Kiev iliharibika kabisa lakini mtawala wa jimbo kwenye mashariki alibaki akaanzisha utemi wa Moscow ulioendelea na kuwa nchi ya Urusi. Sehemu za magharibi ziliingizwa katika milki za Poland na Lithuania.
Leo hii nchi za Urusi, Ukraine na Belarus zinajitazama kama warithi wa Rus ya kihistoria.