Papa Silvester III
From Wikipedia, the free encyclopedia
Papa Silvester III (alifariki 1063) alikuwa Papa kuanzia tarehe 13 au 20 Januari hadi mwezi Machi 1045[1] baada ya Papa Benedikto IX kufukuzwa madarakani mnamo Septemba 1044. Alitokea Roma, Italia[2].
Jina lake la kuzaliwa lilikuwa Yohane Crescenzi.
Alilazimishwa kujiuzulu akafuatwa na Papa Benedikto IX aliyekuwa mtangulizi wake.