Papa Martin I
From Wikipedia, the free encyclopedia
From Wikipedia, the free encyclopedia
Papa Martin I alikuwa Papa kuanzia tarehe 5 Julai 649 hadi kifodini chake tarehe 16 Septemba 655[1]. Alitokea Todi, Umbria, Italia[2].
Alimfuata Papa Theodor I akafuatwa na Papa Eugenio I.
Baada ya kuwa balozi wa Papa Theodori I huko Konstantinopoli, alichaguliwa kuwa mwandamizi wake bila kibali cha kaisari wa Dola la Roma Mashariki.
Kwa kuwa katika Mtaguso wa Laterano (649) na baada yake alipinga uzushi ulioungwa mkono na kaisari Konstans II, wa kwamba Yesu alikuwa na utashi wa Kimungu tu, bila ule wa kibinadamu, hatimaye katika kanisa kuu la Roma akakamatwa na kupelekwa Konstantinopoli kama mfungwa, halafu uhamishoni sehemu za Ukraina kusini, alipofariki baada ya miaka miwili ya mateso[3].
Ndiyo sababu tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu mfiadini.
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.