Pamfilia
From Wikipedia, the free encyclopedia
Pamfilia (kwa Kigiriki: Παμφυλία, Pamphylía [1] kwa maana ya mchanganyiko wa watu [2]) lilikuwa eneo kusini mwa Asia Ndogo, katikati ya Lycia na Kilikia. Kaskazini kulikuwa na Pisidia, ambayo chini ya Warumi ilihesabiwa kama sehemu ya Pamfilia kutokana na wakazi kuwa na asili moja.
![Thumb image](http://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/2/2d/Nympheaum_of_Hadrian_%28Perge%29_02.jpg/640px-Nympheaum_of_Hadrian_%28Perge%29_02.jpg)
![Thumb image](http://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/5/52/15th_century_map_of_Turkey_region.jpg/640px-15th_century_map_of_Turkey_region.jpg)
![Thumb image](http://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/5/58/Stater_slinger_Aspendos_MBA_Lyon.jpg/640px-Stater_slinger_Aspendos_MBA_Lyon.jpg)
Eneo hilo la rasi ya Anatolia (leo nchini Uturuki) lilikuwa kati ya bahari ya Mediteranea na Milima ya Taurus kama mkoa wa Antalya leo.
Ni kati ya maeneo yaliyojinjilishwa na Mtume Paulo pamoja na Barnaba.