![cover image](https://wikiwandv2-19431.kxcdn.com/_next/image?url=https://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/9/9f/Megachile_lagopoda_1.jpg/640px-Megachile_lagopoda_1.jpg&w=640&q=50)
Nyuki mkata-majani
From Wikipedia, the free encyclopedia
Nyuki wakata-majani (kutoka Kiing. leafcutter bees) ni nyuki wadogo hadi wakubwa sana wa jenasi Megachile ya family Megachilidae katika familia ya juu Apoidea ya oda Hymenoptera wanaokata vipande vya majani wanayotumia kupamba viota vyao. Hata hivyo, sio spishi zote za jenasi hii hukata majani. Baadhi hutumia sandarusi kufunga vijumba vya kizazi na kwa hivyo huitwa nyuki-sandarusi. Spishi za jenasi Trachusa vilevile hukata majani lakini hutumia sandarusi pia. Megachile ina spishi nyingi, zaidi ya 1500[1], zinazotokea duniani kote. Afrika ya Mashariki ina spishi takriban 100.
Maelezo zaidi Uainishaji wa kisayansi, Ngazi za chini ...
Nyuki mkata-majani | ||||||||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
![]() Megachile lagopoda (angalia chavua kwenye tumbo) | ||||||||||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||||||||
| ||||||||||||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||||||||||||
Spishi >100 katika Afrika ya Mashariki: Angalia matini | ||||||||||||||||||||||
Funga