Mwili wa nyuki. A: Kichwa B: Toraksi (kidari) C: Fumbatio.
1: Gena (shavu) 2: Verteksi (paji) 3: Oselli (macho sahili) 4: Papasio 5: Jicho tata 6: Ndevu 7: Kinywa 8: Mguu wa mbele 9: Femuri (paja) 10: Mguu wa kati 11: Ukucha 12: Tarsi 13: Tibia (goko) 14: Mguu wa nyuma 15: Sterno 16: Mwiba 17: Ubawa wa nyumba 18: Ubawa wa mbele
Spishi inayojulikana hasa ni nyuki-asali (Apis mellifera) ambaye hufugwa kila mahali duniani. Kuna spishi zaidi ya 20,000 zinazojumlishwa na biolojia kati ya nyuki lakini ni wale wa jenasi Apis wanaotengeneza asali inayovunwa kwa matumizi ya binadamu.