![cover image](https://wikiwandv2-19431.kxcdn.com/_next/image?url=https://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/1/18/Miryam.jpg/640px-Miryam.jpg&w=640&q=50)
Nazareti
mji katika Israeli; inayokaliwa zaidi na raia Waislamu-Waarabu wa Israeli; kitovu cha hija ya Kikristo kama nyumba ya utoto ya Yesu / From Wikipedia, the free encyclopedia
Nazareti (الناصرة kwa Kiarabu, נצרת kwa Kiebrania) ni mji wenye watu 77,445[1] upande wa kaskazini wa nchi ya Israeli, ambao kihistoria unajulikana kama Galilaya.
![Thumb image](http://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/1/18/Miryam.jpg/640px-Miryam.jpg)
Wakazi wengi ni raia wa Israeli wanaoongea Kiarabu na kufuata dini za Uislamu (68,7%) na Ukristo (31,3%).
Nazareti unajulikana kama mji walipokulia Bikira Maria na mwanae Yesu Kristo, ambaye kadiri ya Injili, ingawa alizaliwa Bethlehemu, alikuwa anatajwa kama Mnazareti.