Muskat
From Wikipedia, the free encyclopedia
Maskat (Kiarabu: مسقط) ni mji mkuu pia mji mkubwa wa Omani. Mji una takriban wakazi 650,000.
Kwa maana nyingine, tazama Muskat (maana).
Ukweli wa haraka Nchi, Mkoa ...
Jiji la Muskat | |
Mahali pa mji wa Muskat katika Omani |
|
Majiranukta: 23°36′31″N 58°35′31″E | |
Nchi | Omani |
---|---|
Mkoa | Maskat |
Funga
Maskat ina historia ndefu. Tangu karne ya 2 ulijulikana kama bandari ya biashara ya kimataifa hasa ya uvumba.
Mwaka 1507 ulivamiwa na Wareno waliokaa hadi kufukuzwa mwaka 1649 na Sultani bin Saif. Baadaye mji ulishambuliwa na Waajemi pia na Waarabu Wahabiyya lakini Sultani Sayyid Said alifaulu kutetea utawala wake. Sayyid Said alihamisha baadaye mji mkuu wake kwenda Zanzibar. Tangu wakati huo mji ulirudi nyuma.
Serikali ya Sultani Qaboos bin Said iliweza kuboresha maisha ya wananchi tangu mwaka 1970 hasa kutokana na mapato ya mafuta ya petroli. Mji wa Maskat ulianza kukua na kupanuka sana.