München
From Wikipedia, the free encyclopedia
München (kwa Kibavaria: Minga; kufuatana na uzoefu wa lugha ya Kiingereza Munich; tamka: Munik) ni mji mkubwa wa tatu nchini Ujerumani (baada ya Berlin na Hamburg) na mji mkuu wa jimbo la Bavaria lililopo kusini mwa Ujerumani.
Uko kando ya mto Isar takriban mita 500 juu ya UB.
Idadi ya wakazi ni 1,320,000, lakini rundiko la jiji lina wakazi milioni mbili na nusu.
München ni kati ya vitovu muhimu vya uchumi, utamaduni na sayansi vya Ujerumani.
Klabu ya soka ya Bayern München imeshinda mara 19 kombe la kitaifa na mara tatu kombe la Ulaya.