Muhutwe
From Wikipedia, the free encyclopedia
Muhutwe ni kata ya Wilaya ya Muleba katika Mkoa wa Kagera, Tanzania, yenye postikodi namba 35505 [1].
Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi wa kata walihesabiwa kuwa 12,073 [2]. Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 11,491 waishio humo.[3].
Wakazi wa Muhutwe wanaishi kwa kutegemea shughuli za kilimo na ufugaji. Chakula kikuu ni ndizi. Wanalima kahawa kama zao la biashara.
Muhutwe kwa upande wa magharibi inapakana na mto wa kudumu unaoitwa Mto Ngono. Pamoja na kuwa na uwezekano mkubwa wa kukuza uchumi wa wananchi wanaouzunguka bado fursa hii haijatumiwa ipasavyo kwani mpaka sasa mto huo hauna shughuli zozote za maendeleo, ila ni kivutio kikubwa cha utalii kutokana na kuwa na wanyama wakubwa kama kiboko.