Mtumiaji:KevRobbSW/sandbox
From Wikipedia, the free encyclopedia
Barraba ni kijiji katika mkoa wa New England huko New South Wales, Australia. Kijiji kilikuwa kijiji kikuu cha manispaa ya Barraba Shire lakini kijiji na manispaa yake ziliungamanishwa katika manispaa ya Tamworth Regional Council (Kiswahili: Halmashauri ya Mkoa wa Tamworth) mnamo 2004. Barraba kiko katika Bundarra-Barraba Important Bird Area (Kiswahili: Eneo Muhimu kwa ndege wa mwitu za vijiji Bundarra na Barraba) ambayo inalinda makazi ya ndege ambayo ni nadra Anthochaera phrygia (Kiingereza: Regent Honeyeater).
Barraba | |
Majiranukta: 30°22′42″S 150°36′38″E | |
Nchi | Australia |
---|---|
Majimbo | New South Wales |
Manispaa | Tamworth Regional Council |
Idadi ya wakazi (2016) | |
- Wakazi kwa ujumla | 1,410[1] |
Tovuti: (Kiingereza) barraba.com.au |
Barraba ni km 477 kaskazini magharibi kutoka Sydney, km 548 kusini magharibi kutoka Brisbane, na km 90 kaskazini kutoka Tamworth, ambao ni mji karibu zaidi. Mto wa Manilla unapita kando ya kijiji. Barraba kiko kwenye barabara ya watalii Fossickers Way (Kiswahili: Njia ya Watafutaji wa metali ya thamani na mawe za dhamana) na kijiji kiko kwenye Nandewar Range (Kiswahili: Milima ya Nandewar) kwa urefu wa m 500.