![cover image](https://wikiwandv2-19431.kxcdn.com/_next/image?url=https://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/5/53/Brisbane_Skyline.jpg/640px-Brisbane_Skyline.jpg&w=640&q=50)
Brisbane
From Wikipedia, the free encyclopedia
Brisbane ni mji mkubwa wa tatu wa Australia na mji mkuu wa jimbo la Queensland katika kaskazini ya nchi. Idadi ya wakazi ni mnamo 1,730,000. Iko kando la mto Brisbane na mdomo wake unapita mjini.
![Thumb image](http://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/5/53/Brisbane_Skyline.jpg/640px-Brisbane_Skyline.jpg)
Brisbane ulianzishwa 1824 kama makazi ya wafungwa waliopelekwa Australia kutoka Uingereza. Watu huru walikubaliwa wajenge nyumba hapa tangu 1842. Jina la mji limetokana na gavana yake ya kwanza Sir Thomas Brisbane.
Wakati wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia Brisbane ilikuwa makao makuu ya jenerali Douglas MacArthur aliyeongoza mashambulio dhidi ya Japani.