Mto Godavari
From Wikipedia, the free encyclopedia
Chanzo | Milima ya Ghat ya Magharibi, Maharashtra |
Mdomo | Ghuba ya Bengali |
Nchi | Uhindi, majimbo ya Maharashtra, Chhattisgarh, Telangana, Andhra Pradesh, Odisha |
Urefu | km 1,465 |
Kimo cha chanzo | m 920 |
Tawimito upande wa kulia | mito ya Nasardi, Darna, Pravara, Sindphana, Manjira, Manair, Kinnerasani |
Tawimito upande wa kushoto | mito ya Banganga, Kadva, Shivana, Purna, Kadam, Pranahita, Indravati, Taliperu, Sabari |
Mkondo | m3 |
Eneo la beseni | km2 |
Miji mikubwa kando lake | Nashik, Nanded, Rajahmundry |
Godavari ni mto mrefu wa pili zaidi nchini Uhindi baada ya Ganga. Chanzo chake kiko katika Milima ya Ghat ya Magharibi katika jimbo la Maharashtra [1]. Kutoka huko, karibu na pwani ya magharibi ya Uhindi, mto unaelekea mashariki kwa km 1,465 ukivuka majimbo ya Maharashtra ( 48.6% za njia yake), Telangana (18.8%), Andhra Pradesh (4.5%), Chhattisgarh (10.9%) na Odisha (5.7%). Mwishoni unaingia katika Ghuba ya Bengali.[2]
Beseni lake lina eneo la km² 312,812, ambayo ni kati ya mabeseni makubwa zaidi kwenye Bara Hindi[3].
Mto huo umeheshimiwa katika maandiko ya Kihindu kwa milenia nyingi na unaendelea kutazamwa kama "mto mtakatifu" na Wahindu wengi wanaofika huko kusali.
Katika miongo iliyopita, mto huo umezuiwa na idadi ya mabwawa na malambo yanayochelewesha mtiririko wake. Delta ya mto inalisha watu wengi, wako watu 729 / km 2 - ambayo ni karibu mara mbili kuliko wastani wa kitaifa, na msongamano huo mkubwa umeongeza hatari ya mafuriko. [4] [5]