Ganga (mto)
From Wikipedia, the free encyclopedia
Ganga (Kisanskrit गङ्गा, gaṅga) ni mto mkubwa katika Uhindi wa Kaskazini. Mto una uefu wa 2,511 km unapita nchi za Uhindi na Bangla Desh (Asien).
Ukweli wa haraka Mto Ganga (Ganges) ...
Mto Ganga (Ganges) | |
---|---|
| |
Chanzo | barafuto ya Gangotri |
Mdomo | Ghuba ya Bengali |
Nchi za beseni ya mto | India, Bangladesh |
Urefu | 2,510 km |
Kimo cha chanzo | 7,756 m |
Kiasi cha maji kinachotolewa mdomoni | 14,270 m³/s |
Eneo la beseni (km²) | 907,000 km² |
Funga
Chanzo chake ni katika milima ya Himalaya inapokutana mito ya Alaknanda na Bhagirathi. Kutoka hapa inaendelea kuelekea kusini-mashariki hadi tambarare ya Bengali. Nchini Bangla Desh inaunganika na mto Brahmaputra na kuwa na delta kubwa hadi kuingia katika Bahari Hindi.