![cover image](https://wikiwandv2-19431.kxcdn.com/_next/image?url=https://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/a/a5/Tambacounda_in_Senegal.svg/langsw-640px-Tambacounda_in_Senegal.svg.png&w=640&q=50)
Mkoa wa Tambacounda
From Wikipedia, the free encyclopedia
Mkoa wa Tambacounda ni mkoa mmojawapo wa Senegal. Zamani ikijulikana kama Sénégal Oriental (Senegal ya Mashariki).
![Thumb image](http://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/a/a5/Tambacounda_in_Senegal.svg/640px-Tambacounda_in_Senegal.svg.png)
![Thumb image](http://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/4/45/Map_of_the_departments_of_the_Tambacounda_region_of_Senegal.png/640px-Map_of_the_departments_of_the_Tambacounda_region_of_Senegal.png)
Mkoa una eneo la kilomita za mraba 42,364 lililokaliwa na wakazi 681,310 wakati wa sensa ya mwaka 2013.[1] Mkoa una mipaka ya kimataifa na Mali, Guinea na Gambia.
Eneo lake lilikuwa sehemu ya Milki ya Mali kabla ya kuchorwa kwa mipaka ya kikoloni iliyotenganisha Mali na Senegal.
Tambacounda ni mkoa mkubwa zaidi nchini Senegal, lakini ina wakazi wachache na uchumi wake uko nyuma ya mikoa mingine. Wilaya ya Kédougou ilitenganishwa na Tambacounda mwaka 2008 na kuwa mkoa wa pekee.