From Wikipedia, the free encyclopedia
Mkoa wa Sikasso (kwa Kibambara: Sikaso Dineja) ni mkoa uliomo kusini mwa Mali. Unapakana na nchi za Guinea, Cote d'Ivoire na Burkina Faso.
Mkoa huo una eneo la kilomita za mraba 70,280. Wakati wa sensa ya mwaka 2009 ulikuwa na wakazi 2,625,919.
Mji mkuu wa mkoa huo ni Sikasso ambayo ni mji wa pili kwa ukubwa nchini humo. Sikasso inazidi kukua kwa kasi kutokana na watu wanaokimbia ghasia huko Cote d'Ivoire upande wa kusini.
Makabila makubwa ni pamoja na Wasenufo wanaojulikana kwa vinyago vyao, Wasamago wanaojulikana kwa kuwa wakulima bora wa Mali, na kabila kuu nchini Mali ambao ni Wabambara.
Uchumi wa eneo hilo unategemea kilimo na Sikasso inajulikana kwa matunda na mboga. Mkoa wa Sikasso hupokea mvua nyingi kuliko eneo lingine lolote la Mali.
Mkoa wa Sikasso umegawanywa kwa wilaya (cercles) saba : [1] [2]
Jina la Cercle | Eneo (km2) | Idadi ya watu
Sensa ya 1998 |
Idadi ya watu
Sensa ya 2009 | |
---|---|---|---|---|
Bougouni | 20,028 | 307,633 | 459,509 | |
Kadiolo | 5,375 | 130,730 | 239,713 | |
Kolondiéba | 9,200 | 141,861 | 202,618 | |
Koutiala | 8,740 | 382,350 | 575,253 | |
Sikasso | 15,375 | 514,764 | 725,494 | |
Yanfolila | 9,240 | 163,798 | 211,824 | |
Yorosso | 5,500 | 141,021 | 211,508 | |
Sehemu ya kusini-magharibi ya mkoa wa Sikasso inajulikana kama Wassoulou . Eneo hili ni maarufu kwa muziki wake wa kipekee na utamaduni wa uwindaji. Mji mkuu wa Wassoulou ni Yanfolila .
Koutiala katika sehemu ya kaskazini ya Mkoa wa Sikasso ni kitovu cha tasnia ya pamba nchini Mali.
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.