From Wikipedia, the free encyclopedia
Mopti (kwa Kibambara: ߡߏߕߌ ߘߌߣߋߖߊ, Moti Dineja) ni mkoa wa Mali wenye eneo la km2 79,017. Mji mkuu wake ni Mopti.
Wakati wa mzozo wa mwaka 2012 kaskazini mwa Mali, mpaka kati ya maeneo ya Mali yaliyodhibitiwa na serikali kuu na maeneo ya waasi katika kaskazini ulipitia Mkoa wa Mopti. [1]
Mkoa wa Mopti umepakana na Mkoa wa Timbuktu upande wa kaskazini, Mkoa wa Segou upande wa kusini-magharibi, na Burkina Faso upande wa kusini mashariki.
Wakati wa sensa ya mwaka 2009 idadi ya wakazi katika mkoa ilikuwa 2,037,330. Eneo hili lina makabila mbalimbali yakiwa pamoja na Wabozo, Wasonghai, Wadogon, Wafulani, Wamalinke na Wabambara.
Mto Niger unavuka eneo hilo. Kwenye mji wa Mopti unapokea maji ya tawimto lake Bani.
Maeneo makuu ndani ya mkoa ni pamoja na delta ya barani ya mto Niger karibu na Mopti, miamba ya Bandiagara na uwanda wa Bankass kwenye mpaka wa Burkina Faso. Mlima Hombori wenye kimo cha mita 1153 ni mlima mkubwa nchini Mali ukiwa karibu na Mopti mjini.
Kwa upande wa tabianchi mkoa wa Mopti unachukuliwa kuwa sehemu ya ukanda wa Sahel.
Miji mikubwa zaidi ya eneo hilo ni Mopti, Sevare (ambayo iko ndani ya manisipaa ya Mopti), Djenne, Bandiagara, Bankass, Douentza, na Youwarou .
Uwanja wa ndege wa Mopti unahudumia mkoa wote, wakati Mto Niger una usafiri wa maji hadi Koulikoro na Segou kuelekea magharibi na Timbuktu na Gao upande wa mashariki.
Mkoa huu una umwagiliaji wa kutosha na kilimo chake kimeendelezwa vizuri. Uvuvi ni tawi muhimu la uchumi. Kuna utalii kwenye nchi ya Dogon na hasa katika miji ya Mopti na Djenne penye Msikiti Mkuu wa Djenne ambayo ni jengo kubwa ya udongo duniani.
Mji wa Djenne na Miamba ya Bandiagara zimepokelewa kazika orodha ya Urithi wa Dunia ya UNESCO .
Mopti imegawanywa kwa wilaya (cercles) 8 zinazojumuisha halmashauri 108: [2]
Jina la Cercle | Eneo (km2) | Idadi ya watu
Sensa ya 1998 |
Idadi ya watu Sensa ya 2009 |
---|---|---|---|
Bandiagara | 10,520 | 237,139 | 317,965 |
Benki | 9,054 | 195,582 | 263,446 |
Djenné | 4,563 | 155,551 | 207,260 |
Douentza | 23,481 | 155,831 | 247,794 |
Koro | 10,937 | 267,579 | 361,944 |
Mopti | 7,262 | 263,719 | 368,512 |
Ténenkou | 11,297 | 127,237 | 163,641 |
Youwarou | 7,139 | 81,963 | 106,768 |
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.