Mfalme Yehu
From Wikipedia, the free encyclopedia
Mfalme Yehu (kwa Kiebrania יֵהוּא, Yēhû, maana yake: "YHWH ni mwenyewe"[1] ) alikuwa mfalme wa kumi wa Israeli baada ya Yeroboamu I.
Ni maarufu kwa kuangamiza ukoo wa Ahabu ili kuokoa imani ya Mungu pekee iliyokaribia kutoweka kwa juhudi za malkia Jezebeli. Hivyo alikamilisha kazi ya manabii Elia na Elisha.
Hata hivyo Biblia inamlaumu kama waandamizi wote wa Yeroboamu I kwa kuvumilia mahekalu mbadala ya Betel na Dan.
Alikuwa mwana wa Yehoshafati,[2] na mjukuu wa Nimshi.
William F. Albright alikadiria ufalme wake kudumu miaka 842–815 KK, wakati E. R. Thiele alikadiria miaka 841–814 KK.[3]
Chanzo kikuu cha historia yake ni Kitabu cha pili cha Wafalme, sura 9-10.