From Wikipedia, the free encyclopedia
Melkisedek (kwa Kiebrania מַלְכִּי־צֶדֶֿק, Malkī-ṣeḏeq, yaani "Mfalme wangu ni haki") alikuwa mfalme wa Salemu, Kanaani, katika karne ya 19 KK.
Ni maarufu hasa kwa sababu sura ya 14 ya Kitabu cha Mwanzo katika Biblia ya Kiebrania inasimulia alivyompongeza na kumbariki Abrahamu aliporudi mshindi kutoka vitani.
Humo anatambulishwa pia kama kuhani wa El Elyon ("Mungu Aliye Juu") aliyemtolea sadaka ya mkate na divai.
Hatimaye Abrahamu alimgawia sehemu ya kumi ya mateka yake.
Habari hiyo ikawa hoja kwa wafalme wa Yerusalemu kuanzia Daudi ya kutetea mamlaka yao katika mambo ya ibada (Zab 110:4), ambayo Torati iliwaachia Walawi, hasa wa ukoo wa Haruni.
Hatimaye Waraka kwa Waebrania unazungumzia kirefu habari hizo ili kutetea ukuhani mkuu wa Yesu Kristo, Mwana wa Daudi[1].
Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu, hasa tarehe 26 Agosti[2][3].
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.