Mchikichi
From Wikipedia, the free encyclopedia
Mchikichi (Elaeis guineensis) ni kati ya miti iliyo muhimu zaidi kiuchumi. Matunda yake huleta mawese ambayo hutumika sana kama mafuta ya kupikia, kwa ajili ya madawa mbalimbali na siku hizi pia kama diseli.
Maelezo zaidi Uainishaji wa kisayansi ...
Mchikichi (Elaeis guineensis) | ||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||
|
Funga
Mti unakua hadi kimo cha m. 30. Matunda yake ni madogo yakiwa pamoja kwa shingo. Jumla ya mti mmoja laweza kufikia 50 KG. Matunda haya huharibika haraka hivyo ni muhimu kuyashughulika mara moja baada ya mavuno.
Asili yake Mchikichi ni Afrika ya Magharibi. Mti huu ulipewa jina la kisayansi "Elaeis guenesis" kwa sababu kiasili ilipatikana kwa wingi katika nchi za kanda ya Guinea. Siku hizi inakuzwa zaidi katika Amerika na hasa Asia ya kusini.