![cover image](https://wikiwandv2-19431.kxcdn.com/_next/image?url=https://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/f/f0/St._Maron.jpg/640px-St._Maron.jpg&w=640&q=50)
Maroni
From Wikipedia, the free encyclopedia
Maroni (kwa Kiaramu ܡܪܝ ܡܪܘܢ, Mar|Mār(y) Mārōn; kwa Kiarabu: مار مارون) alikuwa padri mkaapweke mwenye juhudi za sala, lakini pia za umisionari nchini Siria.
![Thumb image](http://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/f/f0/St._Maron.jpg/640px-St._Maron.jpg)
Alifariki kati ya mwaka 406 na mwaka 423 akaanza mara kuheshimiwa kama mtakatifu. Wakristo wengi walihamia kwenye kaburi lake na ndio mwanzo wa tapo la kiroho lenye jina lake ambalo lilizaa nchini Lebanon Kanisa la Wamaroni lililomo katika ushirika kamili na Kanisa la Roma na Kanisa Katoliki lote duniani.
Kuanzia karne ya 17, sikukuu yake inaadhimishwa tarehe 9 Februari[1].