Marashi
From Wikipedia, the free encyclopedia
Marashi (kutoka kitenzi chenye asili ya Kiarabu "kurasha"; kwa Kiingereza "perfume") ni mchanganyiko wa mafuta na manukato yanayonukia vizuri ambayo hupulizwa au kupakwa katika mwili, nguo, viatu au hata nyumba. Marashi hufanya kunukia vizuri hata pahala palipokuwa pakinuka vibaya.
Maandishi ya kale na yaliyovumbuliwa na wasomi wa akiolojia yaonyesha kwamba utumiaji wa marashi umekuwako kwa muda mrefu sana.
Utumiaji wa marashi ya kisasa ulianza katika karne ya 19 baada ya kutengenezwa kwa vitu kama vanilin na coumarin.