Malo
From Wikipedia, the free encyclopedia
Malo (pia: Maclou, Maloù, Mac'h Low, Maclovius au Machutus[1] ; Llancarfan, Glywysing, Wales, 520 hivi - Archambiac, Akwitania, leo nchini Ufaransa, 15 Novemba 621) alikuwa mmonaki nchini kwake, chini ya binamu yake Samsoni wa Dol[2], halafu askofu mmisionari wa Aleth huko Bretagne[3].
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 15 Novemba[4].