From Wikipedia, the free encyclopedia
Makrina Mdogo (Kaisarea wa Kapadokia 330 hivi - Ponto 369), binti Bazili Mzee na Emelia wa Kaisarea, alikuwa mwanamke mwenye ujuzi wa Biblia aliyeishi upwekeni kama mmonaki hadi kifo chake, akawa mfano mzuri ajabu wa mtu mwenye hamu na Mungu asiyevutiwa tena na malimwengu[1].
Alipewa jina hilo kwa heshima ya bibi yake, Makrina Mkubwa, ambaye anaheshimiwa kama mtakatifu pamoja na wajukuu wengine kama Bazili Mkuu, Gregori wa Nisa na Petro wa Sebaste.
Mwenyewe pia anaheshimiwa na madhehebu mbalimbali kama mtakatifu bikira.
Ee Bwana, wewe umetuondolea hofu ya kifo.
Mwisho wa maisha yetu hapa umeufanya mwanzo wa uzima wa kweli.
Kwa kitambo tu utaacha miili yetu ilale usingizi, halafu kwa tarumbeta ya mwisho utaiamsha kutoka usingizini.
Wewe unaukabidhi udongo ukutunzie udongo wako huu ulioufinyanga kwa mikono yako; nawe utauchukua tena na kutoka fungu la kufa, lisilo na muundo, utaugeuza kuwa na uzuri usiokufa.