Magdalena wa Nagasaki
From Wikipedia, the free encyclopedia
Magdalena wa Nagasaki (|長崎のマグダレナ|Nagasaki no Magudarena) alikuwa mtawa wa Kanisa Katoliki kutoka Nagasaki, Japani, ambaye alifia dini yake mjini huko tarehe 16 Oktoba 1634 akiwa na umri wa miaka 23 baada ya kuning'inizwa siku 13 miguu juu na kichwa chini ndani ya shimo lililofunikwa kwa mbao [1].
Wazazi wake walitangulia kufia dini mwaka 1620 hivi.
Papa Yohane Paulo II alimtangaza mwenye heri mfiadini tarehe 18 Februari 1981 na mtakatifu tarehe 18 Oktoba 1987.
Sikukuu yao huadhimishwa tarehe 28 Septemba, lakini ya kwake mwenyewe tarehe 15 Oktoba[2].