Mafuta ya wakatekumeni
From Wikipedia, the free encyclopedia
Mafuta ya wakatekumeni (kwa Kilatini: Oleum Catechumenorum) ni mafuta yaliyobarikiwa yanayotumiwa na Wakristo wa madhehebu mbalimbali (kama Wakatoliki, Waorthodoksi, Waorthodoksi wa Mashariki, Wakatoliki wa Kale n.k.) kabla ya kumpa mtu sakramenti ya ubatizo ili kumuimarisha katika mapambano ya kiroho yanayodaiwa na maisha ya Kikristo.