Madrasa ya Ben Youssef
Ukumbusho wa kihistoria mjini Marakesh, Moroko / From Wikipedia, the free encyclopedia
Ben Youssef Madrasa inayofahamika pia kwa majina ya Bin Yusuf au Ibn Yusuf Madrasa [1]) ni madrasa ya kiislamu iliyopo huko Marrakesh,nchini Morocco. Hivi sasa inatumika kama eneo la kihistoria na madrasa hii ndiyo madrasa kubwa zaidi kwa ukubwa nchini Morocco. [2] Madrasa hii iliitwa kwa jina la Ben Youssef lililotokana na msikiti wa Ben Youssef uliotengenezwa na Sultan Ali ibn Yusuf aliyekua kiongozi kuanzia mwaka 1106 - 1142. [2]